Monday, December 10, 2012
Kanisa la TAG Manzese
Kanisa la muda la TAG lililopo tarafaya Kilosa mijini kitongoji cha Manzese likiwa tayari kwa ajili ya kuanza kutumiwa na waumini wa mahahli hapo. Nilizungumza na mchungaji wa mahali hapo Mch Mwakiame naye aliniambia kwamba katika kazi ya uchungaji ugumu unaojitokeza wakati wa kuazisha kanisa ni kuhusiana na upatikanaji wa kiwanja. Yeye pamoja na waumini wenzake walianzia huduma katika madarasa ya shule ya msingi Sinai iliyopo karibu na kanisa hilo na baadae Mungu amewakumbuka na kuwapatia kiwanja hicho ambapo sasa nuru mpya ya matumaini imeonekana kwa kuwa sasa wanaamini kwamba kanisa litasimama. Aidha Mchungaji huyo anawaomba watu wenye mapenzi mema na shauku ya kutaka kuona kazi ya Mungu ikisonga mbele kuwasiliana naye kupitia namba yake ambayo ni 0654866554 au 0768235397 au 0686977560 kwa ajili ya kuchangia chochote kile kinachoweza kusaidia ujenzi wa kanisa jipya linalotarajiwa kujengwa wakati wakiendelea kuabudu katika kanisa hili la muda. Haya kazi hiyoooo ukiwa na sement, mabati, mbao, viti vya plastiki au fedha ...ni vema basi ukapanda hazina yako hapa na Mungu atakubariki sana...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Allways best comments are those done in wisdom