Tuesday, November 16, 2010

JE MUNGU YUKO?

Watu wengi katika ulimwengu huu  ama ambao hawajaamini kabisa habari za Mungu hata wakati mwingine wale ambao wamekwishaanza kuamini habari za Mungu wakati mwingine wanakuwa na mashaka kuhusu uwepo wa Mungu mwenye nguvu JEHOVA. Uchunguzi unaoyeshakuwa watu wanakuwa na mashaka juu ya uwepo wa Mungu kwa sababu ya siri ya ukuu wa Mungu ambao umejificha na kwamba pengine watu wangetamani wamwone akizungumza na watu ana kwa ana na pia ashushe nguvu zake zionekane wazi kwa kila mtu kama yeye ni MWANGA, basi watu wamuone akishuka kwa mng'aro mkubwa angani mara anapozungumza nasi. Lakini yote hayo yamebakia katika siri ya ukuu Wake. Ilitokea mara chache sana hapo zamani katika kipindia cha akina Musa Mungu ambako Mungu alizungumza na Musa uso kwa uso ingawa Musa hakuweza kuuhimili utukufu wake hadi siku moja alipikutana na Mungu mliimani alishuka aking'aa sana  na macho yake yakashindwa kuona mwanga kwa muda  kwa  sababu ya utukufu wa Mungu.
Hata siku moja Waisraeli wakawa wamekosa kuamini juu ya Mungu wao mwenye nguvu ambaye wamekuwa wakimtumikia, na hii ilimfanya Musa awe na wasiwasi kupeleka maneno ambayo Mungu alikuwa akiimtuma hata akamtaka Mungu afanye jambo la uthibitisho naye Mungu akamjibu Musa siku moja kwamaba kawaambie MIMI NIKO AMBAYE NIKO NIMEKUTUMA. Ikiwa na maana kwamba Yuko na ataandelea kuwepo.( Yuda 1:24 maandiko yanasema tena kuwa Mungu yuko na utukufu uko na yeye milele yote.) 

Ukweli ni kwamba jinsi ambavyo Dunia inakwenda na taratibu zake ambazo hazijawahi kukosewa hata siku moja zikabadilika kama vile, jua kuangaza mchana, mwezi kuangaza usiku na wala hajawahi kutokea jua likakosea na  kuaangaza usiku wa manane, inaonyesha wazi kabisa kwa mtazamo na uelewa wa kawaida kabisa wala haihitaji shule yoyote hapa kwamba yoko mmoja mwenge nguvu anayeongoza taratibu hizi za Dunia. Huyo ndiye Mungu mwenye nguzu tunayemzungumzia katika blog hii. Huyo ndiye kila mtu angependa kufanya urafiki na yeye. Tafiti zinaonyesha wapo miungu wengi Duniani wapatao zaidi ya mia moja ambao wafuasi wamekuwa wakiwaabudu na kuwapatia heshima. Kati ya miungu wote waliopo haijapata hata mmoja wao aliyeweza kufukia UWEZO NA UKUU kama MUNGU JEHOVA NIKO AMBAYE NIKO, Muumba Wa Mbingu, Nchi, Bahari na vyote vinavyoonekana.

Sababu hii imempendeza MUNGU blog hii ya Injili dawa iwepo hewani ili kila mtu mwenye mapenzi mema ya kutaka kutambua uwepo wa Mungu na nguvu zake awe huru kuuliza, kuchangia, kujifunza na kutoa maoni Kibiblia katikablog hii ya wote wenye mapenzi mema.

Eee MUNGU MWENYE NGUVU TUNAKUSIHI IBARIKI Blog HII KWA MAPENZI YAKO WENYE KUKUTAFUTA WAKUONE NA KUPONYWA NAFSI ZAO. Amen

No comments:

Post a Comment

Allways best comments are those done in wisdom