Usemi usemao mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache bado umezidi kuendelea kuwa dhahiri ingawa vyuo vya mafunzo ya Biblia vinazidi kuzalisha watumishi na watenda kazi katika shamba la BWANA. Hawa wanaoneka katika picha ni baadhi ya waumini wa kanisa moja huko maeneo ya Kibaoni Wilayani Kilosa ambao wapo hawana mchungaji yapata sasa mwaka mmoja.
Nilipata nafasi ya kufika huko na kuwahudumia neno la MUNGU nilipata kujifunza mambo ya ajabu. Kwani ingawa kati ya waumini hao wote ambao wengi ni akina mama na hakuna hata mmoja wao amepata bahati ya kujua kusoma imekuwa kazi kwao kujifundisha maneno ya Mungu. Hata hivyo walieleza pamoja na kwamba kina wanapokutana wanaimba tu na kuomba kisha wakajiondokea makwao, bado wataishi kwa njia hiyo hiyo na hawako tayari kumwacha YESU alisema mmoja wao hata kufa. Nilizungumza na mwangalizi wa Section hiyo Kilosa Mch Augustini Lubagula na akakiri kuwepo na upungufu wa watumishi ambao wana utayari wa kufanya kazi ya BWANA katika mazingira magumu ingawa maeneo haya wengi wanayafananisha na nchi yenye maziwa na asali.
Mungu ni mwema sana
ReplyDelete